Katika kuadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwa chama cha ushirika wa akiba na mikopo chuo kikuu cha Dodoma (UDOM SACCOS LTD), uongozi umeandaa bonanza la michezo litakalohusisha wanachama, viongozi, watendaji, pamoja na wadau wote wa UDOM SACCOS LTD. Lengo likiwa ni kuonesha mshikamano, mchangamano na afya bora kupitia michezo, sambamba na kutoa burudani kwa jamii.
MICHEZO ITAKAYOSHINDANIWA NI: -
I. Mpira wa miguu
II. Netiboli
III. Kukimbia
IV. Kuvutana kwa Kamba
V. Mchezo wa bao la Kiswahili
VI. Kukimbia na Magunia
VII. Kufukuza Kuku
VIII. Mpira wa Wavu
IX. Rede
X. Kupanga Glass
XI. Drafti
XII. Kucheza karata
Bonanza hili litafanyika tarehe 10/1/2026 katika viwanja vya michezo CIVE – UDOM kuanzia saa 12:00 Asubuhi hadi saa 7:00 Mchana, pia kutakuwa na supu, nyamachoma na huduma nyingine. Ewe mwana michezo Wasiliana nasi kupitia nambari 0752085279 Wanachama na wadau wote mnakaribishwa sana kushiriki Bonanza hili “UDOM SACCOS LTD,
"Kwa Pamoja Tunatimiza Malengo Yako"