Akiba ni kiasi cha fedha kinachowekwa na wanachama kwa ajili ya kujenga uwezo wa chama kukopesha wanachama wake. Pia akiba inaweza kutumika kama dhamana ya mkopo na inaweza kupunguzwa kwa maombi maalum
Hakuna Kiwango cha juu cha kuweka akiba ila itategemea uwezo na nia ya mwanachama kutumia kikamilifu mazao mengine ya huduma za kifedha.
Akiba za kawaida zitapata Gawio kulingana na taratibu zilizopo na kwa kufuata kanuni ya ushiriki wa mwanachama mwenye kutumia aina za huduma za akiba zinazotolewa. Hata hivyo mbali na kiwango kitakachotokana na ushiriki wa mwanachama, malimbikizo ya Akiba ya kawaida yatazaa faida kwa kiwango cha riba ya asilimia tatu hadi tano (3% hadi 5%) kwa Mwaka. Riba hii itatolewa mwisho wa mwaka baada ya taarifa ya ukaguzi wa hesabu na kupitishwa na Mkutano Mkuu.
Akiba inaweza kuhamishwa na kutumika kufuta deni la mkopo ambao haujarejeshwa pamoja na riba juu ya mkopo uliosalia wakati wa kujitoa uanachama.