Hisa za Mwanachama ni sehemu ya umiliki wa mtaji wa UDOM SACCOS ambayo inamilikiwa na Mwanachama lakini haitakiwi kuzidi asilimia ishirini (20) ya hisa zote za UDOM SACCOS. Hisa hutumika kama kigezo kikuu kwa Mwanachama kunufaika na bidhaa za Mikopo
Utaratibu na Manufaa ya kuwekeza Hisa
- Kila mwanachama ana wajibu wa kumiliki angalau Hisa Sitini (60) zenye thamani ya Tsh. 600,000 na kuhakikisha zinakamilishwa ndani ya Mwaka mmoja ili kukuza mtaji wa UDOM SACCOS.
- Kila Hisa itakuwa na thamani ya shilingi elfu kumi (10,000/=). Kiwango hicho kitabadilishwa na Mkutano Mkuu kulingana na mahitaji ya UDOM SACCOS.
- Hisa zitapata gawio baada ya hesabu za UDOM SACCOS kukaguliwa na kuonesha ziada na kupata idhini ya Mkutano Mkuu, baada ya kutoa matengo ya kisheria.
- Kiwango cha kuchangia hisa kila mwezi kisiwe chini ya thamani ya hisa moja ambayo ni shilingi elfu kumi (10,000/=).
- Kila mwanachama atapewa Hati ya Hisa ya kuonyesha uhalali wa umiliki wake, idadi na thamani ya Hisa anazomiliki pale atakapokamilisha umiliki wa kiwango cha juu cha hisa.
- Mwanachama hataruhusiwa kuhamisha wala kuchukua Hisa zake mpaka unachama wake utakapokoma ambapo atapaswa kukabidhi hati ya umiliki wa Hisa na kulipwa stahiki yake ya Hisa.