UDOM SACCOS LTD TUNATOA MIKOPO YA AINA MBALIMBALI AMBAYO ITAMSAIDI MWANACHAMA KUKAMILISHA SHUGHULI ZAKE ZA KILA SIKU IKIWA NI PAMOJA NA BIASHARA ZAKE, ELIMU NA KUMUWEZESHA KATIKA VIPINDI VYA SIKUKUU NA MATATIZO YA GHAFLA. MIKOPO HIYO NI KAMA IFUATAVYO
Mkopo wa maendeleo:
- Mkopo huu unajumuisha shughuli zote za kimaendeleo kama vile ujenzi, biashara n.k
- Mkopo huu unatolewa mara tatu ya akiba atakayokuwa nayo mwanachama |
- Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 30,000,000/=
- Riba ya mkopo ni 1% kwa mwezi (12% kwa mwaka)
- Muda wa juu wa marejesho ya mkopo wa maendeleo ni miezi 60 (miaka mitano)
- Mwanachama akichukua mkopo wa maendeleo atakatwa gharama zifuatazo kutoka katika mkopo;-
- Ada ya mchakato wa mkopo 1% ya mkopo
- Mfuko wa majanga 1% ya mkopo (gharama hii inasimama kama Bima ya mkopo endapo mwanachama atafariki au kupata ulemavu wa kudumu fedha hizi zitafidia mkopo wa mwanachama husika)
- Ada ya fomu Tsh 5,000/=.
Mkopo wa dharura:
- Mkopo huu unatolewa kwa mwanachama pindi atakapo pata dharura kubwa, na unatolewa kila siku.
- Mkopo huu unatolewa mara tatu ya akiba atakayokuwa nayo mwanachama.
- Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 4,000,000/=
- Riba ya mkopo ni 10% ya mkopo mzima.
- Muda wa juu wa marejesho ya mkopo wa dharura ni miezi 18.
- Mwanachama atapaswa kuja bank statement ya mitatu ya hivi karibuni.
Mkopo wa ChapChap:
- Mkopo huu unatolewa kwa mwanachama pindi atakapo pata dharura ndogo, na unatolewa kila siku.
- Mkopo huu unatolewa mara tatu ya akiba atakayokuwa nayo mwanachama
- Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 500,000/=
- Riba ya mkopo ni 5% ya mkopo mzima.
- Muda wa juu wa marejesho ya mkopo wa chapchap ni miezi 5.
- Mwanachama atapaswa kuja bank statement ya miwili ya hivi karibuni.
Mkopo wa Sikukuu:
- Mkopo huu unatolewa kwa mwanachama kipindi cha sikukuu za kidini kama Pasaka, Eid, Christmas na Maulud.
- Mkopo huu unatolewa kwenye sikukuu za kidini tu ( Krismasi, Pasaka, Eid ma Maurid).
- Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 500,000/=
- Riba ya mkopo ni 5% ya mkopo mzima.
- Muda wa juu wa marejesho ya mkopo wa chapchap ni miezi 5.
- Mwanachama atapaswa kuja bank statement ya miwili ya hivi karibuni
Mkopo wa elimu:
- Mkopo huu unatolewa kwa mwanachama kwaajili ya kulipia ada na gharama zingine za shule.
- Mkopo huu unatolewa mara tatu ya akiba atakayokuwa nayo mwanachama
- Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 2,000,000/=
- Riba ya mkopo ni 11% ya mkopo mzima.
- Muda wa juu wa marejesho ya mkopo wa elimu ni miezi 12(mwaka mmoja)
- Mwanachama akichukua mkopo wa elimu atakatwa gharama zifuatazo kutoka katika mkopo;-
- Ada ya mchakato wa mkopo 1% ya mkopo
- Ada ya fomu Tsh 5,000/=