Kikokotoo cha Mikopo

Michango
Mchango wa kujiunga
Mchango wa Hisa
Mchango wa Akiba
Mchango wa Amana
Kuhusu UDOM SACCOS LTD

UDOM SACCOS LTD ni chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo kinachojumuisha wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma pamoja na waliowahi kufanya kazi katika Chuo Kikuu Cha Dodoma na kuhamishwa/kuhamia kwenye taasisi nyingine za kiserikali, ambapo chama hiki kilianza mchakato mwaka 2009 wa uanzishwaji wake, mchakato huo ulikamilika na kuweza kupata usajiri wake wa kudumu kwa Mrajisi wa vyama vya ushirika mwaka 2011 kwa hati ya DOR 715.

Chama hiki kilisajiliwa rasmi na kupewa cheti cha usajiri na Tume ya maendeleo ya ushirika mnamo tarehe 05/01/2011 Rasmi kuanza huduma mwaka 2013 baada ya kupata viongozi wake kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi wa vyama vya ushirika ,chini ya sheria ya vyama vya ushiri-ka ya mwaka 2003 kikiwa na malengo ya kujikwamua kiuchumi na kujiongezea kipato kwa wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma. Shughuli za chama chetu zikiwa ni kupokea Akiba za wanachama pamoja na kutoa mikopo nafuu kwa wanachama wake, ili kuweza kuwakwamua kiuchumi pale wanapokuwana mahitaji. Shughuli hizi hutolewa katika Chuo kikuu Cha Dodoma Ndaki ya sanaa za kompyuta na mawasiliano.

Dira

Kutoa huduma za kifedha kwa hali ya ubora na toshelezi kwa wanachama wake kwa riba nafuu ili kuwa SACCOS bora inayoongoza nchini Tanzania.

Dhamira

Kufuatilia na kutumia fursa zilizopo katika kujenga mtaji wa ndani kwa kutoa huduma bora kwa gharama nafuu.

Lengo

Malengo yetu ni; Huduma bora na kumjali Mwanachama, Ubunifu na Weledi, Ushirikiano na Utawala bora, Udhibiti wa majanga.

Shughuli

Mwelekeo ukiwa ni kufuatilia na kutumia fursa zilizopo kwa kujenga mtaji wa ndani kwa kutoa huduma bora kwa gharama nafuu.
Wanachama
Mtaji
B
Mali
B
Mikopo
B