Haki za Mwanachama

    Mwanachama atakuwa na haki zifuatazo:
  1. Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano yote inayohusika;
  2. Kushiriki katika kutoa uamuzi wa mambo mbalimbali katika Mikutano Mikuu;
  3. Kupiga kura chini ya misingi ya mtu mmoja kura moja bila kujali idadi ya Hisa anazomiliki;
  4. Kuchagua na/au kuchaguliwa katika Uongozi wa chama.
  5. Kuwa na haki sawa kuhusu mali ya Chama na kudhibiti ipasavyo matumizi yake;
  6. Kupatiwa huduma zozote zinazotolewa na chama ilimradi amekidhi masharti yanayoambatana na huduma hiyo;
  7. Kupatiwa taarifa mbalimbali za shughuli za chama, muhtasari wa mkutano na nyaraka nyingine za chama kwa ajili ya mapitio akiwa katika ofisi za chama;
  8. Kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na Kanuni zake pamoja na masharti haya;
  9. Kuteua Mrithi;
  10. Kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya Bodi ya Uongozi na Mkutano Mkuu;
  11. Kupokea gawio na faida nyingine kutoka katika shughuli za chama kwa kuzingatia masharti; na
  12. Kupewa kitabu cha akiba au kifaa kingine chenye makusudi hayo.