Historia ya Chama

Utangulizi


UDOM SACCOS LTD ni chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo kinacho jumuisha wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma,wafanyakazi wa UDOM SACCOS pamoja na wale waliowahi kufanya kazi katika Chuo Kikuu Cha Dodoma na kuhamishiwa/kuhamia kwenye taasisi nyingine za kiserikali.

Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Chuo Kikuu cha Dodoma, kilianza mchakato mwaka 2009 wa uanzishwaji wake, mchakato huo ulikamilika na kuweza kupata usajiri wake wa kudumu kwa Mrajisi wa vyama vya ushirika mwaka 2011 kwa hati ya DOR 715.

Chama hiki kilisajiliwa rasmi na kupewa cheti cha usajiri na Tume ya maendereo ya ushirika mnamo tarehe 05/01/2011 Rasmi kuanza huduma mwaka 2013 baada ya kupata viongozi wake kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi wa vyama vya ushirika ,chini ya sheria ya vyama vya ushirika ya mwaka 2003 kikiwa na malengo ya kujikwamua kiuchumi na kujiongezea kipato kwa wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma.

Wanachama waanzilishi


UDOM SACCOS ilikuwa na na wanachama waanzilishi 61 tu, ambao wote ni wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma, wakiwemo na watendaji wote wa chama.