Maombi ya kujiunga katika chama yatafuata utaratibu ufuatao: -
-
Mtu yeyote atakayekuwa ametimiza sharti Na.10 ataomba uanachama kwa kujaza fomu iliyoandaliwa na Chama.
-
Mwombaji atajadiliwa na bodi ili kujiridhisha iwapo inakidhi vigezo vya kuwa mwanachama na Bodi inaweza kumkubali au kumkataa.
-
Pendekezo la Bodi ya Uongozi litapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu kwa uthibitisho ambapo waombaji wote waliokubaliwa na Bodi wanayo haki ya kuhudhuria Mkutano Mkuu huo na kujadiliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu na uamuzi wa Mkutano Mkuu utakuwa wa mwisho;
-
Mwombaji atakapokubaliwa na Bodi atatakiwa kulipa kiingilio na Hisa na baada ya kupokelewa na Mkutano Mkuu atatakiwa kutia saini yake au kuweka dole gumba katika daftari la wanachama mbele ya wajumbe wa Bodi wawili;