Mkopo wa maendeleo

Mkopo huu unajumuisha shughuli zote za kimaendeleo kama vile ujenzi, biashara n.k

  • Mkopo huu unatolewa mara tatu ya akiba atakayokuwa nayo mwanachama
  • Kiwango cha juu cha mkopo huu ni Tsh 30,000,000/=
  • Riba ya mkopo ni 1% kwa mwezi (12% kwa mwaka)
  • Muda wa juu wa marejesho ya mkopo wa maendeleo ni miezi 60 (miaka mitano)
  • Mwanachama akichukua mkopo wa maendeleo atakatwa gharama zifuatazo kutoka katika mkopo;-
  • Ada ya mchakato wa mkopo 1% ya mkopo
  • Mfuko wa majanga 1% ya mkopo (gharama hii inasimama kama Bima ya mkopo endapo mwanachama atafariki au kupata ulemavu wa kudumu fedha hizi zitafidia mkopo wa mwanachama husika)
  • Ada ya fomu Tsh 5,000/=