Mwanachama wa UDOM SACCOS

    Mtu yoyote anaweza kujiunga na chama endapo atakidhi mahitaji ya Fungamano la pamoja la uanachama na sharti awe na sifa zifuatazo; -
  1. Awe mwenye umri wa miaka isiyopungua 18.
  2. Awe mwenye tabia nzuri, mwaminifu na mwenye akili timamu
  3. Awe amelipa kiingilio, hisa za uanachama na kuweka akiba kwa kiwango kilichowekwa kwa mujibu wa masharti haya na awe tayari kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za chama.
  4. Awe anaelewa na kuwa tayari kutekeleza madhumuni ya chama kama yalivyoainishwa kwenye masharti haya na kufafanuliwa katika nyaraka mbalimbali.
  5. Awe tayari kufuata masharti ya chama, kanuni na sheria za vyama vya ushirika wakati wote.
  6. Asiwe na shughuli yoyote ile inayofanana na kuweka au kukopesha wanachama ili kuondoa mgongano wa masilahi.
    Wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha UDOM SACCOS watatokana na: -
  1. Wale wote walioshiriki katika mchakato wa uanzilishi na kuomba kuandikishwa kwa chama na ambao wametimiza masharti ya uanachama kwa mujibu wa Masharti haya; na
  2. Wale wote watakaojiunga na chama baada ya kukubaliwa na Bodi na kupitishwa na Mkutano Mkuu.