Wajibu wa mwanachama utakuwa ni pamoja na: -
-
Kukamilisha kununua hisa na kuweka akiba kwa kuzingatia Masharti ya chama;
-
Kufuata na kutekeleza Sheria ya Vyama vya Ushirika na Kanuni zake, Masharti ya chama, maamuzi ya Mkutano Mkuu na maelekezo mengine halali kwa mujibu wa Sheria za nchi;
-
Kurejesha mkopo kwa wakati uliopangwa;
-
Kutoa michango mbalimbali katika kuendeleza madhumuni ya chama kadri itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu;
-
Kubeba dhamana endapo janga lolote litakipata chama;
-
Kuwa mwaminifu na kuonesha ushirikiano katika kutekeleza shughuli za chama;
-
Kumdhamini mkopo mwanachama mwenzake isipokuwa kwamba mwanachama aliyedhamini hatakuwa na haki ya kudhaminiwa na mwanachama aliyemdhamini katika kipindi kile kile;
-
Kulipa mkopo alioudhamini endapo mdhaminiwa/mkopaji atashindwa kulipa mkopo wake; na
-
Kuhudhuria semina na mafunzo yanayotolewa na Chama.